The House of Favourite Newspapers

Niyonzima Awa Mdogo, Aiangukia Simba SC

Haruna Niyonzima

KIUNGO wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima imeelezwa kuwa ameuangukia uongozi wa klabu hiyo kwa kuandika barua ya kuomba msamaha na wakati wowote kuanzia sasa atajiunga na timu.

 

Niyonzima alishindwa kujiunga na kikosi cha Simba kwenye kambi ya nchini Uturuki katika maandalizi ya msimu huu kutokana na tofauti aliyokuwa nayo na uongozi wa klabu hiyo ambapo kwa sasa wameshamalizana.

 

Kiungo huyo ambaye alijiunga na Simba akitokea Yanga msimu wa 2017/18, alishindwa kupata nafasi kubwa ya kucheza msimu uliopita kutokana na kuwa majeruhi.

 

Habari za uhakika ni kuwa tayari Niyonzima amewasilisha barua ya kuomba msamaha na uongozi unalifanyia kazi suala hilo ambapo suala lake limepelekwa katika Kamati ya Maadili ya Simba.

Stori Khadija Mngwai, Championi Ijumaa

Comments are closed.