The House of Favourite Newspapers

Niyonzima awashiwa taa nyekundu Yanga SC

0

NIYONZIMANEW4Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima.

Nicodemus Jonas, Dar es Salaam
MUDA wowote, lolote linaweza kumtokea kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima ikiwemo kupigwa panga klabuni hapo baada ya uongozi wa klabu hiyo kuchoshwa na tabia yake ya kuchelewa kila anapokwenda kwao Rwanda.

Yanga wametangaza kuchukua hatua yoyote ile iwe mbaya ama nzuri kwa wanachama lakini wakitaka kulinda heshima ya klabu kwani nyota huyo ameonekana kushindwa kulinda nidhamu yake kama mchezaji wa kimataifa, akiwa hajaripoti kikosini siku kumi sasa tangu kumalizika kwa michuano ya Kombe la Chalenji iliyofanyika nchini Ethiopia.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, ameliambia Championi Jumatatu kuwa hakuna mawasiliano yoyote kujua tatizo ni nini kiasi cha kuchelewa kujiunga na wenzake, huku kocha Hans van Der Pluijm akihaha kumsaka kwa njia yoyote pasipo mafanikio.

Dk Tiboroha amekwenda mbali na kusema kuwa mpaka sasa Niyonzima ndiye anaongoza kwa udhuru kila anapokwenda likizo ama kwenye majukumu ya timu ya taifa.

“Imefika wakati na sisi tumechoka. Adhabu ya kumkata mshahara tumekata mpaka tumechoka kwa tabia yake. Niyonzima ana rekodi mbaya, mwanzoni mwa msimu huu alichelewa mwezi mzima akisema alipatwa na msiba, akaitwa timu ya taifa akachelewa wiki nzima kwa kisingizio cha kuoa, leo hii ana siku 50 hayupo kwenye timu.

“Lakini sisi tunahesabu siku 10 za baada ya Chalenji, hajulikani yupo wapi. Angalia mwenzake Jean Mugiraneza (Azam) amerejea na jana (juzi Jumamosi) amecheza mechi. Juuko Murshid (Mganda) wa Simba karudi, ni yeye tu hajarudi na hakuna taarifa yoyote,” alifunguka Tiboroha.

Leave A Reply