The House of Favourite Newspapers
gunners X

Niyonzima: Chirwa Anastahili Kuwa Mchezaji Bora

0
Straika wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa

BAADA ya straika wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Oktoba katika Ligi Kuu Bara, kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima, amesema tuzo hiyo imefika sehemu iliyostahili.

 

Chirwa ambaye aliifungia Yanga bao la kusawazisha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba Oktoba 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, katika kuwania tuzo hiyo, amewashinda Erasto Nyoni wa Simba na Ibrahim Ajibu wa Yanga.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Niyonzima alisema hafahamu vinatumika vigezo gani kumpata mshindi wa tuzo hizo, lakini Chirwa anafaa kuwa mshindi kwa mwezi huo kwani hata katika mechi dhidi yao alionyesha kiwango kizuri.

Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima.

“Chirwa kupewa uchezaji bora wa mwezi hajapendelewa bali amestahili kwani nimemuona katika mchezo waliocheza dhidi ya Stand United kule Shinyanga alipambana sana pamoja na kufunga bao moja.

 

“Utaona hadi siku hiyo Yanga inaibuka kwa ushindi wa mabao manne mchango wake ulikuwa mkubwa sana pia hata kwenye ‘derby’ yetu aliisaidia sana Yanga,” alisema Niyonzima.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply