The House of Favourite Newspapers

Niyonzima: Mbona mimi ni yuleyule tu

KIUNGO mchezeshaji fundi Mnyar­wanda, Haruna Niyonzima ametaja siri ya kiwango chake kikubwa alichokionye­sha kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita, huku akisisitiza kwamba yeye ni yule­yule wala hajabadilika.

 

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, juzi, Simba ilifaniki­wa kushinda mabao 2-1 huku Niyonzima akiwa gumzo kubwa.

 

Kiungo huyo alitokea benchi katika dakika ya 60 akichukua nafasi ya Mganda, Emmanuel Okwi na kuhusika kwenye bao la pili la ushindi lililofun­gwa na Mzambia, Clatous Chama baada ya kuu­ruka kwa makusudi mpira uliopigwa na John Bocco kabla ya bao hilo kufun­gwa.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Niyonzima alisema aliing­ia uwanjani akiwa ameona upungufu wa wapinzani wao akiwa benchi.

 

Niyonzima alisema, akiwa benchi kocha wake alimpa maelekezo ya nini cha kukifanya pindi aki­ingia na kikubwa alimtaka akae na mpira, kupiga pasi za kwenda mbele ili wapate bao lingine.

 

“Niwaambie tu watu, Niyonzima ni yuleyule wa zamani hana tofauti na huyu wa sasa, kikubwa ni nafasi tu. Nikiendelea kupata nafasi wataniona zaidi,” alisema Niyonzima.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Comments are closed.