The House of Favourite Newspapers

Niyonzima: Tutakachowafanya Stand United Watajuta

0
Haruna Niyonzima.

KIUNGO wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amesema kuwa watahakikisha wanafanya kila liwezekanalo ili kuondoka na alama tatu kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United.

Niyonzima ameyasema hayo baada ya kuishuhudia timu yake ikitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Mbao FC katika mchezo wa ligi hiyo Alhamisi wiki iliyopita kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Akizungumzia mchezo wao ujao ambao watacheza Jumapili hii dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Niyonzima alisema, sare yao dhidi ya Mbao ilikuwa imepangwa.

“Hata kama ukimleta Zidane au nani, kama Mungu ameandika droo inakuwa droo, timu yetu ni nzuri na tuliweza kufunga mabao mawili lakini tulishindwa kuyalinda japo tulitengeneza nafasi nyingi.

“Watu wanatakiwa kukumbuka kuwa, tupo ugenini japo tunafahamu tulitakiwa kushinda lakini hata kuipata hii pointi moja si mbaya,” alisema Niyonzima.

Said Ally, Dar es Salaam.

Leave A Reply