The House of Favourite Newspapers

Niyonzima: Yanga Njoeni Tumalizane

MARA baada ya kiungo mchezeshaji Mnyarwanda Haruna Niyonzima, kukutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Abdallah Bin Kleb ambaye ndiye aliyehusika katika usajili wake akitoka APR ya kwao, kiungo huyo amefunguka kuwa anataka kuivaa jezi ya Yanga kwa mara nyingine.

 

Niyonzima alikutana na Bin Kleb ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya ushindi ya Stars juzi Jumatatu nchini Rwanda wakati ambao kiungo huyo alikuwa anaichezea timu yake ya taifa iliyokuwa ikicheza na Taifa Stars, nchini humo kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Bin Kleb ndiye ambaye alisimamia usajili wa Yanga kwa mara ya kwanza akitua nchini akitokea APR ya kwao Rwanda ambapo alikaa hapo kwa misimu minne kabla ya kuhamia Simba.

Kiungo huyo ambaye kwa sasa anaitumikia AS Kigali ya kwao ameliambia Championi Jumatano, kuwa kwake hana tatizo lolote la kurejea Yanga endapo viongozi wa klabu hiyo watakuwa tayari kumhitaji kutokana na kuamini klabu hiyo ndiyo ambayo ana upepo nayo.

 

“Kwanza nimefurahi kukutana na Bin Kleb kwa sababu yeye ni sawa na baba yangu kwa sababu ndiye ambaye alisimamia usajili wangu wakati ambao natua Tanzania kwa mara ya kwanza.

 

“Lakini pia mimi sina ubaya na Yanga na nipo tayari hata leo kurudi na kuvaa jezi yao kama wakinihitaji kwa sababu naamini huko ni sehemu sahihi kwangu na ndipo nina upepo mzuri napo, kuitu cha muhimu wao waje kisha wazungumze nitakuwa tayari kwa ajili ua kujiunga nao,” alisema Niyonzima.

 

Lakini katika picha ambayo aliitupia kiungo huyo fundi mtandaoni, licha ya uwepo wa kiongozi wa Simba, Haji Manara lakini alimkata kiasi cha mashabiki kuhoji kuwa hakuondoka vizuri klabuni hapo.

Stori na  Said Ally na Wilbert Molandi, Dar

Comments are closed.