Njemba Anaswa na Video 555 za ‘Ngono’ Kwenye Begi

RAIA mmoja wa Colombia ambaye jina lake halikutajwa, ameshikwa na polisi wa Hispania akiwa na video 555 zenye kuonyesha sehemu za siri za wanawake ikiwa ni pamoja na nguo zao za ndani.

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 53 alichukua video hizo jijini Madrid, Hispania, kwa siri akitumia kidude maalum (cellphone) alichokuwa anakiweka chini ya miguu ya wanawake waliokaa au waliosimama, kikachukua taswira ya ndani ya wanawake hao katikati ya miguu yao.

Wanawake waliolengwa ni wale waliokuwa wanasafiri kwenye treniĀ  wakiwa wamekaa au kusimama, na kwenye maduka makubwa (supermarket).

Polisi nchini Hispania wanasema video hizo zilizokuwa zikionyesha taswira za wanawake wakiwemo watoto wadogo zilianza kusambaa mnamo Julai 2018 kwenye tovuti.

Katika njama hizo mtu huyo alipata wafuasi 3,519, watembeleaji 84,594 na kufanya idadi nzima ya watu walioangalia video hizo kufikia 1,367,999.

 

 


Loading...

Toa comment