The House of Favourite Newspapers

Njia 5 Rahisi za Kujitibu Tatizo la Nguvu za Kiume

0

Leo nitazungumzia tatizo linalowasumbua wanaume wengi la upungufu wa nguvu za kiume.

Mfumo wa maisha, umesababisha wanaume wengi kuwa na tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume. Kabla ya kuendelea, ni vizuri tukalichambua tatizo lenyewe la nguvu za kiume na chanzo chake.

Mwanaume anahesabika kuwa na tatizo la nguvu za kiume, endapo atakuwa anawahi sana kumaliza awapo faragha, viungo vyake vya uzazi havikakamai vya kutosha awapo kwenye tendo na akimaliza, hawezi tena kurudia kwa mara nyingine mpaka baada ya muda mrefu kupita.

Tatizo la upungufu wa kiume mara nyingi husababishwa na matatizo ya kimwili au ya kisaikolojia ambapo mwanaume huwa dhaifu wakati wa tendo na wakati mwingine kushindwa kabisa kufanya chochote.

Sababu za kimwili (Physical) zinaweza kuwa ni kwa sababu mishipa ya damu inashindwa kufikisha damu yenye msukumo kwenye viungo vya uzazi. Kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini husababisha mafuta hayo kuganda kwenye kuta za mishipa ya damu na kuzuia damu kutiririka vizuri, tatizo ambalo kitaalamu huitwa atherosclerosis.

Pia wagonjwa wa kisukari nao wapo kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na tatizo hili, pia upungufu wa madini ya Zinc na vitamin pia husababisha tatizo hili.

Sababu za kisaikolojia ni pamoja na kuwa na msongo wa mawazo, hofu, uchovu wa akili au kama mtu aliwahi kukumbwa na tatizo kubwa siku za nyuma ambalo limemuathiri kisaikolojia au kama ana dosari katika mfumo wake wa homoni.

Sababu nyingine zinazoweza kusababisha tatizo hili ni matumizi ya madawa ya kulevya, pombe au kuchanganya vyote viwili kwa pamoja. Uvutaji wa sigara nao ni sababu nyingine ya tatizo hili, pamoja na kuendesha baiskeli kwa muda mrefu.

Wengi wakishagundua wana tatizo hili, huhangaika kwa waganga wa kienyeji au mahospitalini, wengine wakilazimika kutumia dawa kali kama Viagra na nyingine za namna hiyo kujaribu kurudisha heshima kwenye ndoa zao.

Hata hivyo, habari njema ni kwamba unaweza kujitibu mwenyewe tatizo hili.

Zipo mbinu ambazo mwanaume yeyote, hata yule ambaye tatizo lake limekuwa kubwa, anaweza kuzitumia na kurudisha heshima na kujiamini kwa sababu ipo wazi kwamba mwanaume akishakuwa na matatizo ya nguvu za kiume, hawezi kuwa na furaha maishani, hawezi kujiamini wala hawezi kuheshimika na mwenzi wake.

MAZOEZI YA VIUNGO

Mfumo wa maisha umesababisha wanaume wa sasa wawe legelege sana. Ukiwa na mwili legelege, hauwezi kuwa na ‘stamina’ ya kutosha uwapo faragha na mwenzi wako, kwa hiyo jambo la kwanza unalotakiwa kulipigania, ni kuhakikisha unakuwa na ukakamavu.

Si lazima uingie gym kwenda kunyanyua vyuma vizito, ingawa nayo inasaidia lakini unaweza kuweka ratiba ya kufanya mazoezi kila siku. Hata kama unatingwa sana na kazi, jitengee muda, asubuhi au jioni kwa ajili ya mazoezi.

Kama hujawahi kabisa kufanya mazoezi, anza kufanya mazoezi mepesi kama kukimbia kwa dakika zisizopungua thelathini. Mazoezi ya kuruka kamba na kupiga push-ups nayo ni muhimu sana kwa sababu yanakuongezea pumzi na stamina.

Hakikisha mazoezi yanakuwa sehemu ya maisha yako na ukizingatia vizuri ratiba, baada ya wiki mbili tu utaanza kuona mabadiliko ya namna unavyolimudu tendo la ndoa unapokuwa na mwenzi wako. Kadiri siku zinavyosonga mbele, ongeza kiwango na muda wa mazoezi.

VYAKULA

Inashangaza kuona mwanaume anashindia chipsi mayai, soseji na vitu vya mafutamafuta halafu anategemea kuwa ‘fit’ kwenye tendo. Huko ni kujidanganya, mwanaume anapaswa kula vyakula vya kuupa mwili nguvu na nishati. Hebu badilisha vyakula, anza kula ugali wa dona, mbogamboga za majani za kutosha na kunywa maji kwa wingi, utaona mabadiliko.

Ipo orodha ndefu ya vyakula ambavyo vina uwezo wa ajabu wa kukupa heshima uwapo na mwenzi wako, kwa leo nitakutajia vichache.

Vyakula hivyo ni vitunguu swaumu, ndizi mbivu, karanga, kunazi (blueberries), zabibu, mbegu za maboga, tangawizi, mihogo mibichi, supu ya pweza, korosho, madafu, nazi na asali. Siku nyingine nitakufafanulia zaidi namna unavyoweza kupangilia vyakula vyako na ukapata matokeo ya kufurahisha.

KUJIAMINI

Hili nalo ni jambo muhimu sana ambalo kila mwanaume anapaswa kujifunza namna ya kujiamini anapokuwa kwenye maandalizi mpaka kwenye tendo lenyewe. Mwingine unakuta hana tatizo lolote la kiafya lakini kwa sababu akili yake haijatulia, ana hofu kubwa moyoni mwake, hajiamini kama ataweza kukidhi haja za mwenzi wake, anaishia kucheza chini ya kiwango.

Lazima ujue namna ya kujiandaa kisaikolojia na kuishinda hofu kabla na wakati wa tendo na njia nyepesi, hutakiwi kuwa unawaza mambo mengine kichwani. Tuliza akili yako, pumua kwa uhuru ukivuta hewa ya kutosha na kuitoa kwa mdomo. Nitakuelekeza namna ya kujenga kujiamini na ukifanikiwa, utaona matunda yake.

Kwa bahati nzuri, mbinu hizi ukizifuatisha kwa umakini, matokeo yake huonekana haraka na utashangaa uwezo wako ukiongezeka kuliko hata yule anayetumia madawa makali ya kuongeza nguvu za kiume.

Itaendelea wiki ijayo.

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Leave A Reply