Njia kumi kusaidia kupunguza unene-3

obesityTunaendelea kufafanua njia za kupunguza unene:

Kama usipotafuna chakula vizuri au ukila huku unakunywa sana maji au vinywaji vingine, chakula hakimeng’enywi vizuri tumboni.

ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA
Mafuta ni suala muhimu sana mwilini. Ila ulaji wake sharti uwe wa mpangilio. Yaani unaowiana. Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya nguvu, yaani wanga kama vile ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate, mahindi, nk.

NJIA KUMI KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE
Vyakula vya kujenga mwili yaani protini ni mbogamboga na nyama, vyakula vyenye “madini” kama vile mbegumbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi na vya vitamin kama matunda, maziwa, mayai, nk.
Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina ya chuma, hasa nyama nyekundu pia ina protini, nguvu na mafuta. Ila mafuta yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri, huganda.

Kula nyama ya kuku na samaki. Mafuta ya samaki ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega 3 ambayo husaidia mwili na kinga ya maradhi mwilini.
Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za majani (mbichi) na si vizuri kula nyama kila siku. Kama huwezi kukaa bila kula nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili.

Lakini pia tunapendekeza kula mbegu za korosho, karanga au mlozi (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kila siku. Haya ni mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta.

MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO
Mazoezi ni njia sahihi ya kupunguza unene.
Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu na kutokwa jasho kwa wingi kwa hiyo hayo ni mazoezi tosha.

Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti.
Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme na kufanya mapafu na moyo kwenda kasi, viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu.

Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea kwa kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha kama mpira wa miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk; Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili au tatu kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani misuli na mishipa inahitaji kupumzika na kukua.

Kama unapenda kuinua vyuma lazima uwe na mwalimu wa kukuelekeza; na si vizuri kufanya kila siku. Wastani wa mara mbili tatu kwa juma inatosha kabisa.
Wiki ijayo tutaeleza aina mbili ya mazoezi, usikose nakala ya gazeti hili.


Loading...

Toa comment