The House of Favourite Newspapers

NJIA RAHISI ZA KUONDOA KITAMBI

 LEO tutajadili mbinu nne muhimu zitakazokupa mafanikio makubwa katika kupambana kuondoa kitambi.

 

Kwanza jiulize kitambi ni nini? Kitambi ni mafuta ya ziada yanayojikusanya katika sehemu ya tumbo. Hii hutokana na kula chakula kingi na kisicho na ubora, pia kuishi maisha ya kibwenyenye yanayokunyima fursa ya kufanya mazoezi. Mafuta yanayofanya kitambi huweza kujengeka chini ya ngozi, au ndani kabisa ya tumbo yakizunguka viungo kama tumbo, utumbo na ini.

 

Mafuta haya, hususan yale yaliyo ndani ya tumbo ni hatari kwa afya zetu. Ikumbukwe pia kwamba, kitambi huwa na mwonekano wake kutokana na misuli ya tumbo kuwa legelege. Hii husababisha mafuta yaliyo tumboni kuusukuma ukuta wa tumbo kiurahisi hivyo kutengeneza shepu ya mbinuko.

CHAKULA UNACHOKULA

Ni vema ufahamu kila unachofanya na kula. Kuna mpangilio wa chakula wa siku 7, siku 10 na mpaka siku 21. Na mtu anaweza kupungua unene na uzito kuanzia siku tatu mpaka 15 inategemea kama atafuata kwa umakini ushauri na sayansi ya milo.

 

Supu ya kabeji, mlo wa kijeshi ama kwa Kingereza ‘Military Diet’ kwa kula kipande cha mkate wa kahawia, yai kidogo na matunda au mlo wa yai ‘Egg diet’ kwa kula mayai yaliyochemshwa na matunda pamoja na saladi. Hizi ni baadhi tu ya njia za haraka za mpangilio wa chakula au diet ili kupunguza unene kwa haraka zaidi.

 

Kuna wengine wanadhani ili kupunguza kitambi au unene dawa ni kujinyima kula au kushinda na njaa jambo ambalo si sahihi. Madhara ya kujinyima kula ni kukosa viini lishe katika mwili, hali inayosababisha kudumaa na uchakavu wa mwili yaani nuru kupotea kisha kuwa kama mgonjwa.

Si watu wote wanaweza kujinyima kula kwa sababu huwezi kuizuia njaa. Unaweza kupata hatari ya kushuka kwa sukari ghafla au presha ikashuka ghafla kwa sababu ya kukosa viini lishe muhimu. Kujinyima kula ili kupunguza unene au uzito si njia endelevu, huwezi kujinyima milele.

 

Njia nzuri ya kupungua unene na uzito ni kuzingatia ubora wa chakula. Katika sayansi ya mapishi tunaamini kila chakula ambacho tunakiweka mwilini kina muitikio tofauti.

 

Mwili ukiupa sukari na vyakula vya wanga unamimina homoni nyingi za kunenepesha. Lakini ukiupa mayai, samaki parachichi na baadhi ya matunda ambayo yana sukari kidogo kama matango, mwili utaitikia kwa kumwaga homoni ya kunenepesha kwa kiwango kidogo sana.

 

Utapata virutubisho vyote na mwili hautafubaa wala kusinyaa. Hivyo basi hakikisha unapunguza au kuacha kabisa kula vyakula vyenye kutiwa sukari na vinywaji vyenye sukari.

Kula mbogamboga kama vile mchicha, kisamvu, majani ya maboga na matunda kama vile embe, nanasi, parachichi, ndizi, zabibu, machungwa na kadhalika, tena ule kwa wingi wakati ukipunguza kwa kiasi kikubwa vyakula vyenye wanga mwingi kama ugali na wali.

 

Acha kutumia mafuta ya wanyama badala yake tumia mafuta yanayotokana na mimea kama alizeti, michikichi, ufuta, nasi, mbegu za pamba nk. Ukiweza acha kula vyakula vya wanga wakati wa usiku na hakikisha unakula chakula cha usiku angalau saa moja kabla ya kulala.

 

FANYA MAZOEZI

Pamoja na kula tulivyoelekeza hapo juu, hakikisha unafanya mazoezi na unafahamu kwa undani kazi ya mazoezi yako katika mwili wako.

Comments are closed.