The House of Favourite Newspapers

NMB, CARE International zaungana kusaidia vikundi

0

 

nmb (1)

NMB na CARE International zaungana kusaidia vikundi vya kuweka na kukopa

  • Wazindua NMB Pamoja Account mahususi kwa vikundi hivyo

NMB kwa kushirikiana na shirika la kijamii la CARE International jana lilizindua akaunti maalumu ya NMB Pamoja Account kwaajili ya vikundi vya kuweka na kukopa ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa vikihifadhi fedha zao majumbani.

NMB Pamoja Account ni mahususi kwa vikundi vya kuweka na kukopa ambavyo kwa miaka ya hivi karibuni vimekuwa vikiongezeka kwa kasi huku utunzaji wa fedha zao ukikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kuibiwa na hata baadhi ya wanavikundi kula njama na kukimbia na fedha za vikundi na hivyo kupeleka vilio kwa wanavikundi.

nmb (2)

Kwa kutambua hilo, NMB na CARE International wameviunganisha vikundi zaidi ya 300 zenye watu zaidi ya 250,000 lengo likiwa kuviunganisha vikundi zaidi ya 10,000 nchi nzima ndani ya muda mfupi na kuvitengenezea mfumo wa kibenki utakaorahisisha shughuli zao, kuwahakikishia ulinzi wa fedha zao na pia ukuaji wa fedha zao zikiwa benki tofauti na kuziweka kwenye masanduku majumbani.

nmb (4)Kupitia NMB Pamoja Account, wanavikundi watafaidika na mafunzo ya ujasiliamali na elimu ya fedha, fedha zao kuongezeka kwa asilimia 3 kwa mwaka pamoja na uwezo wa kutumia NMB mobile kuangalia salio, tuhamisha salio kutoka akaunti ya kikundi kwenda akaunti nyingine.Pia wanavikundi mmoja mmoja wataweza kuunganishwa na huduma ya NMB Chap Chap Account na hivyo kuwaingiza katika mfumo rasmi wa kutumia taasisi za fedha kuhufadhi na kupata huduma mbalimbali za kifedha.

NMB Pamoja Account ni akaunti mahususi iliyoundwa kutoa huduma kwa mahitaji ya vikundi vya kuweka na kukopa bila kuondoa dhana ya msingi ya uendeshaji inayotumika na vikundi hivyo. Kupitia akaunti hii miamala inafanyika kwa urahisi na wepesi kupitia NMB Mobile baina ya akaunti ya kikundi na akaunti nyingine.

Leave A Reply