NMB Mdhamini Mkuu wa Mashindano ya Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi
Mchezaji wa Golf, Asha Sugira toka Benki ya NMB akiendelea na Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Kombe la Mkuu wa Majeshi nchini “NMB CDF TROPHY” yaliyofanyika katika Viwanja vya Gofu vya Lugalo jijini Dar es Salaam, Oktoba 5/2024. NMB ni mdhamini mkuu wa mashindano haya yaliwakutanisha zaidi yq wachezaji 120 wakiwemo pia kutoka nje ya nchi.