The House of Favourite Newspapers

NMB Wataoa Msaada Kwa Watoto Yatima Dar

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Serikali  pamoja na Makampuni Makubwa wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi  (kushoto) akimkabidhi mtawa zawadi za watoto yatima wa kituo cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, jijini Dar es Salaam.

KUTOA ni moyo na wala siyo utajiri! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya wafanyakazi wa Benki ya NMB kutoa sehemu ya kipato chao na kuwasaidia watoto yatima wa kituo cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi hao wamefikia hatua hiyo ya baada ya kuguswa na changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili watoto katika kituo hicho.

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Serikali pamoja na Makampuni Makubwa wa NMB, Filbert Mponzi, amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo kwa sababu wao ni sehemu ya jamii kwa hiyo wana wajibu wa kutoa kidogo walichonacho na kuwasaidia wenzao wasiokuwa nacho ili waweze kupata mahitaji muhimu katika maisha yao.

 

“Tumeamua kutoa msaada huu kituoni hapa kutokana na kuguswa na matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo watoto katika kituo hiki, lakini pia tumefanya hivyo kwa kituo cha Kurasini kilichopo pia jijini hapa.

“Kwa niaba ya Benki ya NMB  na wafanyakazi kazi wake wote, nichukue nafasi hii kuwaomba Watanzania wengine na makampuni mbalimbali hapa nchini kujiwekea utaratibu wa kuwasaidia watoto yatima kwa kutoa chochote walichonacho,” alisema Mponzi na kuongeza kuwa:

“Misaada tuliyotoa ni chakula, pamoja na nguo.  Utaratibu huu tumekuwa tukiufanya kila mwaka ambapo wafanyakazi wote wa NMB huchangishana fedha na kile kidogo ambacho tunakipata basi hukitoa katika jamii yetu kwa kuwasaidia wale wenye mahitaji maalumu. ”

 

 

Comments are closed.