Benki ya NMB imeanza mwaka kwa kusambaza upendo kupitia kampeni ya #MastaBataKoteKote kwa kumzawadia mshindi wa pikipiki mpya aina ya boxer wa draw ya 6 – Ally Asbat Abdallah kwenye droo ya pili ya mwezi iliyofanyika mkoani Tanga.
Mpaka sasa, kampeni hii imeshawazadia wateja wake jumla ya Sh. Mil 150,500,000 kwa washindi 623 na kabla ya jana, boda boda 9 ziliishanyakuliwa; 7 kwenye droo za wiki na 2 kwenye droo ya kwanza ya mwezi iliyofanyika Iringa. Zikijumulishwa na 2 za jana, jumla inakuwa pikipiki 11 zenye thamani ya zaidi ya 33m/- huku nyingine tatu zikiwa zimebakia kwa ajili ya droo za kila wiki zilizobaki.
Zimesalia siku 25 tu kuelekea grand finale ambapo tutashuhudia wateja 8 wakijishindia safari ya kwenda Dubai kwa siku 4 huku benki ya NMB ikiwalipia kila kitu.
Usiache kadi yako ya NMB mastercard nyumbani kufanya malipo ya matumizi yako au kwa kuscan QR kujiweka katika nafasi ya kuweza kuwa mmoja wa washindi wa #MastaBataKoteKote.