The House of Favourite Newspapers

NMB Yadhamini Semina ya Bloggers

1

Ofisa Uhusiano wa Benki ya NMB, Doris Kilale (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni kumi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii, Joachim Mush (kulia).

2

Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii, Joachim Mushi (katikati) akizungumza na wanahabari.

3

…Doris Kilale naye akizungumza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).

4

Wanahabari wakichukua tukio hilo.

BENKI ya NMB imedhamini semina ya Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii nchini Tanzania maarufu kama ‘Bloggers Network’ (TBN) ambapo imetoa hundi ya shilingi milioni kumi.

Hundi hiyo imekabidhiwa leo na Ofisa Uhusiano wa Benki hiyo, Doris Kilale wakati wa mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam leo alipomkabidhi mwenyekiti wa mitandao hiyo, Joachim Mushi mfano wa hundi ya kiasi hicho.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mushi amesema lengo la semina hiyo inalenga juu ya uendeshaji mitandao ya kijamii,namna ya kuzingatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji.

“Kimsingi lazima tukubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la kusambaza habari mbalimbali tena kwa muda mfupi, hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwapiga msasa wanaoendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii.

“TBN inaamini njia pekee ya kupamabana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ni kuendelea kutoa elimu kwa waendeshaji na watuniaji ili mwisho wa siku wasikubali kutumika vibaya au kuitumia vibaya mitandao hii katika kutoa taarifa,” alisema Mushi.

Naye Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale alisema mchango unaotolewa na mitandao ya kijamii ni mkubwa hivyo wameamua kudhamini semina hiyo ili kuwapa uelewa mpana waendeshaji na wanahabari kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya mitandao hiyo.

“Kitendo cha kujitolea kuwa mdhamini mkuu wa semina hiyo ni hatua kubwa ya kuthamini mchango wa mitandao hiyo katika jamii, NMB inawajali wananchi katika masuala mbalimbali ikiwemo hili la upashaji habari kwa jamii,” alisema Kilale.

Semina hiyo inatarajiwa kufanyika Desemba 5 na 6 mwaka huu ikijumuisha washiriki zaidi ya 150 Kutoka Tanzania nzima na itafanyika katika Ukumbi uliopo Jengo la Golden Jubilee (PSPF) jijini Dar, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Na Denis Mtima/GPL

halotel-strip-1-1

Comments are closed.