The House of Favourite Newspapers

NMB Yasaidia Ujenzi wa Duka Kubwa la Dawa Ruangwa

0

 

nmb

NMB imesaidia ujenzi wa duka kubwa la dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kwa kuchangia kiasi kikubwa cha shs milioni 30. Duka hilo limejengwa na NMB kwa kushirikiana na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na limegharimu kiasi cha sh milioni 59. Hili ni duka la kwanza kudhaminiwa na Benki hiyo huku likikadiriwa kuhudumia vituo vya afya, Zahanati na Hospitali zaidi ya 516 katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma hasa kwa upande wa Wilaya ya Tunduru.

Ujenzi wa duka hilo ni hatua ya mwitikio wa Benki ya NMB kuunga mkono juhudi za Raisi Dk. John Magufuli kwa kuweka maduka ya dawa katika hospitali kubwa nchini ili kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi na kwa bei nafuu.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa duka hilo jana, Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Richard Makungwa alisema NMB ilivutiwa sana na mpango wa serikali kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na benki hiyo imeamua kuunga mkono juhudi hizo za kuhakikisha huduma bora na nafuu zinawafikia wakazi wa Ruangwa na mikoa ya jirani.

NMB

Pichani ni Afisa Mkuu wa wateja wakubwa na serikali wa benki ya NMB – Richard Makungwa akitoa taarifa ya NMB mbele ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania –Majaliwa Kassim Majaliwa katika uzinduzi rasmi wa Duka la Kisasa la Dawa lililopo katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani LIndi. Benki ya NMB imegharamia ujenzi wa Duka hilo kwa kutoa Kiasi cha Shilingi MIlioni 30 huku duka hilo likikadiriwa kutumika na vituo vya afya, zahanati na hospitali zaidi ya 516 za mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma hasa wilaya ya Tunduru.Hafla ya uzinduzi rasmi ilifanyika katika Duka hilo wilayani Ruangwa Juzi.

Akizindua rasmi duka hilo, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa aliipongeza NMB kwa kudhihirisha msemo wa benki hiyo ya kuwa karibu zaidi na Wananchi.

Leave A Reply