The House of Favourite Newspapers

NMB yawafikia wakazi wa Kakonko

1

nmb

Benki ya NMB imefungua rasmi tawi lake jipya wilayani Kakonko. Tawi hili limefunguliwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya.

NMB Kakonko linakuwa miongoni mwa matawi zaidi ya 170 yaliyotapakaa nchini kote na katika kila wilaya bila kujali wilaya ipo pembezoni vipi. Tangu kubinafsishwa mwaka 2005, NMB imekuwa inaongeza matawi zaidi ya 10 kwa mwaka na hivyo kufikia matawi zaidi ya 170 mwaka huu.

Maono ya NMB ni kuhakikisha kuwa huduma za kibenki zinakuwa karibu zaidi ya wananchi na hivyo kuwaingiza watanzania kwenye uchumi rasmi kupitia huduma za kibenki kokote walipo hata kama ni wilaya za pembezoni mwa nchi.

Tawi la NMB Kakonko linatoa huduma zote za kibenki, ikiwa ni pamoja na huduma ya mikopo, kuweka na kutoa fedha, huduma ya fedha za kigeni, kufungua akaunti mbalimbali pamoja na kufanya malipo ya aina yoyote ambayo yanapatikana kwenye tawi lolote la NMB nchini.

Mbali na kufungua tawi la NMB Kakonko, NMB pia ilitoa msaada wa Madawati ya shilingi Milioni 5 kwaajili ya shule za msingi za wilayani hapo na pia vitanda vya hospitali kwaajili ya hospitali ya wilaya ya Kakonko vyenye thamani ya shilingi Milioni 5 hivyo kufanya jumla ya msaada uliotolewa kuwa shilingi milioni 10.

 

1 Comment
  1. Raphael Hokororo says

    Hongera NMB kwa kazi mzuri

Leave A Reply