BAADA ya kuandamwa na mashabiki, mkongwe wa filamu kutoka Nollywood, Anita Joseph ameamua kuanika ukweli kuwa hakuwa na mimba.
Hivi karibuni staa huyo aliweka vipimo vikionesha akiwa na ujauzito wa watoto mapacha ambapo mashabiki wengi walijitokeza na kumpongeza kutarajia kupata watoto wa kwanza.
Akifanyiwa mahojiano na redio moja nchini Nigeria, Anita aliweka wazi kwamba haukuwa ujauzito wake bali wa rafiki yake. “Sina ujauzito.
Rafiki yangu wa karibu alinionesha vipimo vya ujauzito wake wa watoto mapacha. Hakuwa amebahatika kupata mtoto kwa miaka 19 ikanigusa sana nikaweka mtandaoni vipimo hivyo,” alisema Anita.

