The House of Favourite Newspapers

Nonga aikosakosa Stand United

0

DSCF0654 Paul Nonga

Wilbert Molandi,
Dar es Salaam
KAMA zari kwa Stand United, kwani yule mbaya wao Paul Nonga aliyesajiliwa na Yanga hatokuwepo katika mchezo wa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nonga amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh milioni 40, lakini ameuomba ruhusa uongozi wa timu yake mpya akamalize mambo yake kisha ajiunge rasmi na timu hiyo.
Katika mchezo wake wa mwisho akiichezea Mwadui FC, Nonga alifunga bao moja lililoiwezesha timu hiyo kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United. Bao lingine lilifungwa na Fabian Gwanse.
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm aliiambia Championi Jumamosi kuwa, Nonga ameomba ruhusa kwa uongozi kwenda kwao kubeba mizigo na kumalizia mambo mengine ili ahamie rasmi Dar es Salaam.
“Nonga ameomba ruhusa hivyo hatocheza dhidi ya Stand, ameenda kwao kumaliza mambo yake na atarejea Dar es Salaam, Jumapili (kesho) ili Jumatatu aanze na wenzake,” alisema Pluijm raia wa Uholanzi.
Ujio wa Nonga katika kikosi cha Yanga umeongeza idadi ya washambuliaji na kufikia watano, wengine wakiwa ni Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Malimi Busungu na Mateo Anthony.

Leave A Reply