The House of Favourite Newspapers

Nora adaiwa kunasa mimba!

0

NORABrighton Masalu

MSANII wa kitambo katika tasnia ya maigizo na filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ anadaiwa yuko ‘kitumbo ndii’ na ndiyo sababu ya kukaa kimya tena kwa siku za hivi karibuni, Ijumaa linadokeza.

Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar mmoja wa rafiki wa muda mrefu wa Nora ambaye pia ni msanii wa muda mrefu (jina tunalo), alisema kwa sasa Nora anatumia muda mwingi kuwa ndani kutokana na kile alichokiita “kupelekwa mputa” na mimba hiyo aliyodai kuwa changa bila kutaja umri wake.

Baada ya kupata habari hizo Ijumaa lilimtafuta Nora kupitia simu yake ya mkononi, ambapo baada ya kusomewa madai hayo alisema:

“Sasa kama ni kweli kuna ajabu gani juu ya hilo? Kwani mimi ni mwanaume? Mbona unaingilia sana mambo yangu binafsi, achana na mimi bwana,” alisema Nora na kukata simu kabla ya kuizima.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

globalbreakingnews.JPG

Leave A Reply