The House of Favourite Newspapers

NSSF Yatanga Uhakiki Kwa Wastaafu Na Wategemezi Wanaolipwa Pensheni Ya Kila Mwezi

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unawatangazia wastaafu na wategemezi wote wanaolipwa pensheni ya kila mwezi kuwa kutakuwa na zoezi la uhakiki kuanzia Februari 3, 2025 hadi April 30, 2025.

Zoezi hili litafanyika Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 10:30 jioni kwenye ofisi zote za NSSF.
Kwa wastaafu waliopo Zanzibar, uhakiki wao utafanyikia ofisi ya ZSSF Makao Makuu, Unguja na ofisi za ZSSF, Pemba.

Aidha kwa wastaafu waliopo Dar es Salaam, uhakiki wao utafanyika katika ofisi za mikoa ambazo ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Ubungo, Mbezi Beach na Kigamboni.
Kwa wastaafu wazee au wagonjwa wasiojiweza, taarifa itolewe kupitia barua pepe [email protected] au kwa kupiga simu ya bure 0800116773.