The House of Favourite Newspapers

Nuh: Mtoto Kanipa Mzuka Kimuziki!

STORI: IMELDA MTEMA | GAZETI LA IJUMAA | SHOWBIZ

BAADA ya hivi karibuni mkewe kujifungua mtoto wa kike aitwaye, An­yagile, msanii wa Bongo Fleva, Naftar Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amefunguka kuwa, mtoto huyo amempa mzuka zaidi wa ku­fanya muziki.

Akipiga stori na Showbiz, Nuh alianza kwa kufafanua maana ya jina la Anyagile kuwa linamaanisha amenikuta baada ya kumpokea, nguvu kubwa anaielekeza kwenye muziki ili apate chochote cha kum­fanya akue.

“Nimefurahi sana kupata mtoto wa kike, mke wangu alishakuwa kwenye uhusiano na wanaume wengi lakini haja­wahi hata kuwabebea mimba lakini kwa muda mfupi amenipa­tia kijike. Kilichobaki sasa hivi ni toa ngoma weka ngoma,” alisema Nuh anayebamba na Wimbo wa Anamer­emeta.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.