The House of Favourite Newspapers

Nwanko Kanu Alivyoshiriki Uzinduzi wa Safari ya Butiama Kumuenzi Mwalimu Nyerere

0
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Nwanko Kanu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Philip Besiimire wakijiandaa kuanza mbio katika uzinduzi huo.

Mbio za kuelekea Butiama mkoani Mara alipozaliwa muasisi wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ni Baba wa Taifa  zimezinduliwa jijini Dar leo ambapo miongoni wa waliohudhuria tukio hilo ni mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Nwanko Kanu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mtandao wa simu za mkononi ya Vodacom, Philip Besiimire na wadau wengine.
Tukio hilo lilizinduliwa kwa mbio fupi za baiskeli kuanzia Ufukwe wa Coco kuelekea daraja la Tanzanite na kugeuzia Hospitali ya Aghakhan huku wengine wakifika mpaka Sea Cliff na kurudi Coco kumalizia mbio hizo.  Mbio hizo ambapo zimekuwa zikifanyika kila mwaka imeelezwa kuwa lengo lake kuu ni kumuenzi  Baba wa taifa na kuyaenzi mazuri mengi aliyoyafanya. Safari hiyo ya kuelekea Butiama mwaka huu imedhaminiwa na Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Vodacom. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN /GPL                                                       

Leave A Reply