The House of Favourite Newspapers

Nyambizi Yanaswa na Shehena ya Madawa Baharini

NYAMBIZI katika bahari ya Pacific imekutwa ikiwa na zaidi ya dawa za kulevya pauni 12,000 zenye thamani ya dola za Marekani milioni 165 sawa na Tsh bilioni 379.5.

 

Chombo hicho kinachotembea chini ya bahari kilikamatwa na maofisa wa kikosi cha majini wa Marekani, ambapo pia waliwakamata watuhumiwa wanne wa kusafirisha dawa hizo.

Tukio hilo ni moja ya matukio kadhaa ya kukamatwa kwa dawa za kulevya yaliyofanyika mwezi huu, ambapo kikosi cha doria cha majini cha Seneca nacho kilikamata pauni 12,000 za Cocaine Septemba 20, mwaka huu, jijini Miami.

 

Aidha, vyombo viwili vya vikosi vya doria vya majini kutoka Tahima na Midgett pia vilikamata pauni 9,000 za dawa za kulevya mapema mwezi huu.

Comments are closed.