The House of Favourite Newspapers

Nyamwela: Bora Bongo Fleva Kuliko Dansi

0
Super Nyamwela.

MNENGUAJI na mwanamuziki wa Dansi ambaye kwa sasa amegeukia pia Bongo Fleva, Hassan Musa ‘Super Nyamwela’ bendi za muziki wa Dansi amesema kwa sasa hazilipi hivyo amejikita zaidi kwenye muziki wake binafsi.

Akibonga na Showbiz Extra, Nyamwela ambaye hivi karibuni ameachia ngoma inayokwenda kwa jina la Kochokocho yenye mahadhi ya Bongo Fleva Dansi, alisema mkataba wake na bendi anayoifanyia kazi ya The African Stars International ‘Twanga Pepeta’ unamruhusu kufanya kazi zake na sasa amejikita zaidi huko na mafanikio ni makubwa.

“Siku hizi siendi mara kwa mara kwenye bendi maana Dansi sasa hivi hailipi, nimejikita kwenye muziki wa Bongo Fleva na nimeshapata mialiko ya kufanya shoo sehemu mbalimbali kama Muscat, Dubai na Australia hivyo nimeamua kukomaa humuhumu,” alisema Nyamwela.

GLADNESS MALLYA

Irene Uwoya: Napenda Mwanaume Mwenye Sura ya Kiume

Leave A Reply