The House of Favourite Newspapers

Nyoka Mwenye Vichwa Viwili Aitwaye Double Dave

TUMEZOEA kuona nyoka wa rangi tofauti  na wenye maumbo makubwa zaidi duniani, leo tunakuletea nyoka huyo anaejulikana kwa jina Double Dave  mwenye vichwa viwili.

Image result for double dave snake

Nyoka huyo mwenye vichwa viwili aliyepewa jina la Double Dave amepatikana katika msitu mmoja katika jimbo la New Jersey,  Marekani.

And umbo dogo na sumu kali,  ana vichwa viwili vilivyokamilika, macho manne na ndimi mbili ambazo zinafanya kazi tofauti.  Pia ana uwezo wa kujibadilisha na kuvimba anapokutana na adui.

Image result for double dave dave schneider

Bwana Schneider ambaye ni mtaalam wa wanyama wanaotambaa, amesema yeye na mtaalam mwenzake walimwona nyoka huyo  Agosti 25 na wakampa jina la Double Dave kwa sababu yeye Schneider na mwenzake wote majina yao ni David.

 

Comments are closed.