The House of Favourite Newspapers

NYOKA WEUSI WAVAMIA IKULU, RAIS AKIMBIA OFISI

MSEMAJI wa Ikulu ya Liberia amesema rais wa nchi hiyo hivi sasa anafanyia kazi nyumbani kwake baada ya nyoka wawili kugunduliwa wakiwa katika ofisi yake, shirika la habari la utangazaji la Uingereza (BBC) limesema.

 

Naibu Mwandishi wa Habari wa Ikulu, Smith Toby, ameliambia shirika la habari la The Associated Press kwamba aliyekuwa mchawi wa soka kimataifa na ambaye ni Rais wa Liberia, George Weah, ameambiwa kutoingia  katika ofisi yake hadi jengo hilo la Wizara ya Mambo ya Nje lipuliziwe madawa.

 

Weah anategemewa kurejea ofisini Jumatatu ijayo.

 

Nyoka hao ambao ni weusi walionekana wiki hii wakitokea katika shimo kwenye  wa jengo hilo katika eneo la mapokezi.  Liberia ni nchi ambayo ina nyoka wengi wenye sumu, hivyo maofisa wanaohusika na ofisi hiyo wanalichukulia suala hilo kwa umakini ambapo upulizaji wa madawa dhidi ya wadudu na wanyama wa aina zote unafanyika.

 

Weah, aliyekuwa mchezaji bora za shirika la soka duniani (Fifa) mwaka 1995 alikuwa rais wa nchi hiyo tangu Januari 2018.

 

Katika mtafaruku huo, wafanyakazi wameambiwa kutofika kazini hadi Aprili 22.

 

 

Polisi na walinzi wa rais wameonekana wakilinda makazi ya Weah jijini Monrovia, mji mkuu wa nchi hiyo.

 

 

Comments are closed.