The House of Favourite Newspapers

Nyoni: Sasa Waje Wengine

MFUNGAJI wa bao pekee la Simba dhidi ya Yanga, Erasto Nyoni amesema sasa wamesahau juu ya mchezo huo na wanajipanga kwa ajili ya kuwakabili Ndanda FC, kesho Jumapili.

 

Nyoni beki wa zamani wa Azam FC, Jumapili iliyopita aligeuka shujaa kwa timu yake ya Simba baada ya kuifungia bao dakika ya 37 na kuiwezesha kushinda bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Nyoni alisema: “Kwa sasa mchezo na Yanga ndiyo umepita na tunachokiangalia ni namna ya kupata tena matokeo mbele ya wapinzani wetu wengine tutakaokutana nao mbele yetu.

 

“Naamini benchi la ufundi limeona pale ambapo tulikosea na watare-kebisha kwa ajili ya kutufanya tuwe bora zaidi kwenye mchezo ujao wa ligi.

 

“Lengo letu ni moja tu kwamba tunatakiwa kuhakikisha tunapata matokeo yaliyo bora kwenye kila mechi ambayo tutashuka uwanjani na siyo vinginevyo,” alisema Nyoni ambaye hutumika zaidi ya namba moja akiwa uwanjani.

 

Akizungumzia tena kuhusu bao lake alilolifunga dhidi ya Yanga, Nyoni alisema: “Yanga waliwafikiria zaidi John Bocco, Shiza Kichuya na Emmanuel Okwi na waliwalinda wakatu-sahau wengine.

 

“Mimi kwa kuwa sikuwa kwenye malengo yao ya kunilinda ndiyo maana ukaona nimefunga kirahisi.”

Simba yenye pointi 62 kileleni mwa ligi kuu, kesho Jumapili inacheza na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ndanda ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 23.

Stori na Said Ally

Comments are closed.