The House of Favourite Newspapers

Nyoshi: FM Academia Haiwezi Kufa

0

TWANGAPEPETA2Kiongozi wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Nyoshi El-Sadaat

MUSA MATEJA

PREZIDAA wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Nyoshi El-Sadaat amevunja ukimya kwa kusema kuwa pamoja na bendi yao kuondokewa na mkurugenzi wao Martin Kasyanju kamwe haitakufa kama wengi wanavyodhania.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Novemba 17, mwaka huu Nyoshi alisema kumekuwa na hisia mbovu kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo wakihusisha kifo cha aliyekuwa mmiliki wa bendi hiyo na kufa kwa bendi kwamba itasambaratika kwa kukosa usimamizi na uendeshaji uliyo imara, jambo ambalo anasema si kweli kwani bila yeye mambo yataenda vizuri tu.

Screen Shot 2015-03-25 at 2.26.09 PMBendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’

“Ningependa kuwahusia mashabiki wa FM Academia kuwa ni bendi ambayo imejiimarisha kila sekta hivyo haiwezi kusambaratika kwa sababu tu mkurungezi wetu hayupo hai, ninachoweza kusema, watambue bosi Kasyanju aliunda msingi mzuri kwa familia yake juu ya bendi hii hivyo naamini kwa uongozi wa watoto, mkewe na wasimamizi wengine kamwe Ngwasuma haitakuja kusambaratika,” alisema Nyoshi na kuongeza:

“Ninasema hivi kwa kuwa nina kila sababu ya msingi, kwani hapa nilipo kwa sasa nipo Kilosa na timu nzima ya FM Academia tulikuja kupiga shoo na baada ya hapa Ijumaa tutakuwa Dodoma mjini tukifanya yetu ila Jumamosi tutarudi Dar kupiga shoo ya nguvu huko Kigamboni, tayari tumetunga wimbo mpya tulioupa jina la Hombeje ambao ni mahususi kumkumbuka mkurugenzi wetu,” alisema Nyoshi.

Leave A Reply