The House of Favourite Newspapers

Nyota 10 Watemwa Simba SC Kubaki 15 Pekee Kati ya 25

0

Wilbert Molandi, Championi Jumatano, Habari

KLABU ya Simba imepanga kuwabakiza wachezaji 15 pekee kati ya 25 iliowasajili msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (FA). Timu hiyo, inataka kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika watakayoshiriki mwakani.

Wakati wakipanga kuwaacha wachezaji hao, tayari nyota wao muhimu wameshaanza kuaga akiwemo Abdi Banda ambaye mkataba wake umemalizika, wengine ni Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu ambao nao wamemaliza mikataba.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alisema bado hawajapokea rasmi ripoti ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog lakini tayari Kamati ya Utendaji ilikutana kufanya tathmini ya kikosi chao kwa ajili ya usajili.

Hans Poppe alisema wameona wachezaji 10 ambao hawana mchango na kupanga kuwaondoa katika kikosi hicho ambao wapo watakaotolewa kwa mkopo kwa ajili ya kukuza viwango vyao. “Msimu huu tulikuwa na kikosi kipana kilicholeta ushindani na kufanikisha malengo yetu lakini licha ya kuukosa ubingwa, kuna kitu tumeonyesha na kufanikiwa kupata Kombe la FA.

“Katika kuhakikisha msimu ujao wa ligi na mashindano ya kimataifa tunakuwa bora zaidi, tumepanga kuwaacha wachezaji 10 kati ya hawa 25 tuliokuwa nao msimu huu.

“Wakati tukiwaacha hao, tumepanga kuongeza idadi ya wachezaji 10 kati yao tunataka wenye uwezo wa kucheza mashindano ya kimataifa, kama unavyojua mwakani tutaiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo ni lazima tuwe na kikosi imara,” alisema.

Leave A Reply