The House of Favourite Newspapers

Nyota Simba Waapa Kufa Na Wydad Casablanca ya nchini Morocco leo

0

MASTAA wa Simba wameapa kupigana kufa na kupona ili kuhakikisha timu yao inapata matokeo mazuri katika mchezo wao wa ugenini dhidi ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco.

Simba leo Jumamosi watakuwa na kibarua cha kucheza na Wydad Casablanca ambao hawajapata matokeo katika mchezo wowote wa makundi ya michuano hiyo.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Nahodha wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ alisema kuwa, wanatambua ugumu wa mchezo huo kutokana na matokeo mabaya ya mpinzani wao lakini hata kwa upande wao hawajapata matokeo mazuri jambo ambalo linawasukuma na wao kupambana ili kuipa timu ushindi.

“Tunafahamu kuwa wapinzani wetu wapo katika hali mbaya kwa kuwa hawajapata matokeo yoyote ya ushindi kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa hivyo lazima mechi iwe ngumu.

“Hata sisi kwa upande wetu hatujapata matokeo ambayo tuliyataka hivyo lazima tuhakikishe kuwa tunapata matokeo ili tuweze kufika mbali, malengo yetu sio kupoteza mchezo wowote bali ni kushinda,” alisema Tshabalala.

Naye beki wa kulia wa timu hiyo, Shomari Kapombe alisema kuwa: “Haijalishi kwa sasa tutacheza wapi na tunacheza na timu ya aina gani kikubwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa tunapambania alama muhimu katika mazungira yotote.”

TAMBO za ALLY KAMWE KUHUSU PACOME – APIGA HESABU KALI za KUFUZU ROBO FAINALI CAF – AMTAJA KONKON…

Leave A Reply