The House of Favourite Newspapers

Nyota Wanne Simba Waweka Rekodi Ligi Kuu

0

NAHODHA wa Simba, John Bocco anaongoza kwa wazawa wenye mabao mengi ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa nayo tisa kibindoni pia ana pasi mbili za mabao.

 

Namba hiyo ya Bocco inakwenda sambamba na mshikaji wake Meddie Kagere ambaye yeye pia ametupia jumla ya mabao tisa.

Wakati mabingwa hao watetezi wakiwa ni namba moja kwa upande wa kutupia mabao mengi wakiwa nayo 45 pia watengeneza mipango namba moja wanatokea Simba wakiwa na pasi tisa.

 

Luis Miquissone mwenye mabao matatu ana pasi tisa za mabao sawa na Clatous Chama mwenye mabao sita na ana pasi tisa za mabao.

 

Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba ameliambia Championi Jumatanokuwa ushindi ndani ya uwanja unamtegemea kila mchezaji hivyo kila mmoja ana kazi ya kupambana kufanya vizuri.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

Leave A Reply