The House of Favourite Newspapers

NYUMBA YA UDONGO HAIPIGWI DEKI

Image result for nice couples

 HALOOOO eeeehhhh! Umezoea cheko la nyundo ngoja nikupe la msumari miye, nginjha nginjha! Nimeingia mjini tena Anti Naa kungwi wa makungwi we’ endelea kununa tu, ulishindwa kutakata mtoni utatakata bafuni? Hebu nipishe miye tangu lini hodi ya chooni ikakaribishwa? Nashanga’ wee unayelilia uzuri wakati wenzako wanalilia bahati, wangapi wazuri hata bahati hawapati! Heee heeeiyaaaaa! Muwasho wa ulimi, haukunwi kwa kidole bibi weee, upo? Baada ya kukupa udambwidambwi nianze kukupa hiki kilichonifanya leo kuwa hapa! Si unanijua tena Anti Naa sikwepeshi, waswahili wanakwambia raha ya kupanda daladala kusiwe na foleni, uongo?

Shoga nakumbuka sana kipindi cha nyuma niliwahi kuja na mada ya mashuka hapa, nikagundua kuwa wengi wetu tunayachukulia kama mapambo tu wakati kama umefundwa ukafundika unaweza kuyatumia kumpa ishara mumeo, siyo lazima umwambie unatandika tu. Nilielezea rangi zote mwisho nikamalizia rangi mchanganyiko ya shuka, nikawasema sana wale wanaochukulia poa rangi hiyo kuwa ina maana kubwa kama vile kumpa ishara ya usafi mumeo, kama kichaka chake kimejaa au chako basi ni siku ya kufanyia kazi viwanja vyenu vikatakata, halooooo eeeeehhhh!

Leo shoga nataka tuongelee rangi, najua utashangaa kama fundi viatu aliyekuta noti ya elfu moja ndani ya kiatu! Shoga rangi za chumbani zina maana kubwa kuliko unavyofikiria, kama hujawahi basi jaribu shoga yangu kisha utanipa mrejesho! Siku zote nawaambia wanaume wa leo siyo wa jana ati! Mwanaume anahitaji kumfanyia vitu spesho asione kwingine kuna afadhali, uongo?

Tena usiwe kama majani ya chai, hujulikani kama dawa ya ngirau ya kichwa! Shoga chumba kinatakiwa kupambwa kwa taa za rangi hafifu zenye rangi ya kuvutia kama vile kijani, pinki, bluu, zambarau au yoyote ili mradi isiwe na mwanga mkali, upo nyonyo? Kama ulikuwa hujui jua sasa shoga yangu, rangi hizi hafifu ukiwa nazo chumbani zina faida kubwa ya kutunza uhusiano wenu, kwanza ni silaha nzuri sana inayoamsha hisia za huba kwa mumeo kwa sababu zinachangia kumfanya mpenzi wako awe na muonekano wa pekee wenye kuleta hisia zinazokuongezea matamanio.Related image

Pili shoga, mwanga huu hafifu husaidia kupendezesha mavazi kama vile night dress au boksa na kukufanya umuone kama malkia ambaye amekupa fursa ya pekee ya kuwa naye kwa usiku huo. Humfanya mumeo kudeka na kutoa kauli zenye kuvutia zilizojaa maneno matamu. Shoga hebu kuwa mkweli tu, nyumba ya udongo tangu lini ikapigwa deki? Hata ukiishi nyumba ya udongo lazima ujue maandalizi yake ya kuandaa kuanzia juu hadi chini, siyo unakurupuka na dekio unataka kupiga.

Mapenzi ya giza yale ya kimyakimya kama kukimbiza mwizi wa gizani huchangia spidi na hamu kupoa na hivyo mumeo kumaliza kwa muda mfupi unashangaa unajua labda ni nguvu za kiume wakati wewe ndiyo chanzo kwa kutoweka mazingira ya chumba kuwa ya kumvutia! Kwa leo niishie hapa nisije kuonekana naongea sana bure, ni mimi Anti Nasra, Shangingi Mstaafu.

Comments are closed.