The House of Favourite Newspapers

Obama asema Trump hawezi kuwa rais Marekani

0

Barack Obama

Rais Barack Obama.

Rais Barack Obama amesema kuwa anaamini mgombea urais nchini humo kupitia Chama cha Republican, Donald Trump hatakuwa rais wa Marekani.
Amesema kazi hiyo ni “kazi kubwa”.

“Ninaendelea kuamini kwamba Bw. Trump hatakuwa rais. Na sababu ni kwamba nina imani sana na Wamarekani,” amesema Bw. Obama.

Watu hawatampigia kura, alisema Bw Obama, kwa sababu “wanajua kuwa rais ni kazi kubwa”.
“(Kazi hii ) Si kama kuzungumza katika kipindi cha runinga, si matangazo au mauzo ya bidhaa, ni kazi ngumu. Si kazi ya kushawishi watu na kufanya utakalo ndipo utokee kwenye vichwa vya habari siku fulani.”

Bw. Trump amemjibu na kusema ni kama kusifiwa iwapo utakosolewa na rais ambaye ameharibu sana nchi.
Mwanasiasa huyo anamchukia sana Obama na miaka ya nyuma alizoea kumtaka atoe stakabadhi za kuthibitisha kwamba alizaliwa Marekani.

Trump, mfanyabiashara na tajiri mkubwa kutoka New York, anaongoza kwenye kura za maoni katika kinyang’anyiro cha kuteua mgombea wa Chama cha Republican.
30CBF43C00000578-3427713-Second_Republican_presidential_candidate_Donald_Trump_speaks_as_-a-168_1454401699044

Donald Trump.

Tayari ameshinda uchaguzi wa mchujo jimbo moja, na anaongoza kwenye kura za maoni jimbo la South Carolina, ambako wafuasi wa Republicans watashiriki uchaguzi wa mchujo Jumamosi wiki hii.

Akiongea wakati wa mkutano mkuu wa kiuchumi wa nchi za kusini Mashariki mwa Asia unaofanyika katika jimbo la California, rais aliulizwa na mwanahabari kumhusu Trump.

Leave A Reply