RAIS mstaafu wa Marekani Barack Obama aliitumia Siku ya Wakimbizi Duniani kumshutumu Rais wa Marekani, Donald Trump katika sera yake ya kuwatenganisha watoto na familia zao.
Obama aliyasema hayo kupitia mtandao wa Facebook akiuliza iwapo Marekani inakubali ukatili wa kuwatengenisha watoto na wazazi wao.
Aliongeza kwamba: “Tuthibitishe kupitia sera, sheria na vitendo vyetu kwamba tunathamini familia zetu na zingine zote.”
Obama.
Rais Trump amekuwa akiendesha sera ya kuwatenganisha watoto wakimbizi na familia zao hasa wale wanaoingia Marekani, hili limo katika amri aliyosaini karibuni.
Comments are closed.