Odama kumuanika baba wa mtoto soon!
Staa wa filamu Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ Na Suzan Kayogela.
BAADA ya kukataa katukatu kumuanika baba wa mtoto, staa wa filamu Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ kwa mara ya kwanza amesema mwaka mpya na mambo mpya na kuwa sasa yupo tayari kumuanika na soon atajulikana.
Tangu ajifungue mtoto wa kiume, Jason miaka takriban miwili iliyopita, Odama alikuwa akikataa kumuweka wazi baba wa mtoto huyo.