The House of Favourite Newspapers

ODAMA: MUDA WA KUOLEWA BADO

Jennifer Kyaka ‘Odama’

LICHA ya umri kuonekana kuanza kumtupa mkono, muigizaji mkongwe Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amefunguka kuwa, hababaishwi na ndoa ambazo wanafunga baadhi ya mastaa wenzake kwani wakati wake ukifika naye atafunga.  

 

Akizungumza na Amani, Odama alisema hakuna kitu kizuri duniani kama kusubiri wakati wa Mungu ambao ndio sahihi.

 

“Mimi naamini kabisa kila jambo lina wakati wake na wakati mzuri ni wa Mungu anapokuwa amekupangia jambo litatimua, sio tu kukurupuka kwa sababu mwingine kafanya,” alisema Odama. Odama mwenye umri wa miaka 36, tayari amejaaliwa kupata mtoto mmoja na mwanaume ambaye hakumuweka wazi.

Comments are closed.