ODEMBA AKUMBUKA NYUMBANI

Miriam Odemba

MISS my home! Mwanamitindo maarufu ndani na nje ya Bongo, Miriam Odemba ametoa la moyoni kuwa akili yake kwa sasa amekuwa akiwaza nyumbani Tanzania hivyo kukosa raha.  

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa kwa njia ya simu akiwa nchini Ufaransa, Odemba alisema kuwa hata mtu akae nchi za watu kwa miaka mingi, lakini bado picha ya nyumbani haifutiki akilini.

 

“Siyo kwamba hakuna maisha mazuri au sipati ninachotaka, lakini siku zote nyumbani kuna ladha yake. Nimekumbuka sana nyumbani na kungekuwa karibu kwa kweli kila wakati wangeniona,” alisema Odemba ambaye tayari amefungua taasisi yake hapa nchini ya Run With Odemba

Stori: Imelda Mtema, Dar

Loading...

Toa comment