ODEMBA KUIBUKA SIKU YA WANAWAKE

Miriam Odemba

MWANAMITINDO maarufu ndani na nje ya Bongo, Miriam Odemba anatarajia kuwa mmoja wa wanawake watakaohudhuria katika Onesho la Tanzanite Women Forum and Lunch linalotarajiwa kufanyika Machi 9, mwaka huu ambayo ni siku ya wanawake duniani litakalofanyika katika Hoteli ya Double Tree jijini Dar.

 

Akistorisha na Gazeti la Ijumaa, Odemba alisema kuwa anafurahia sana kuwa mmoja wa wanawake waliopata mualiko maalum katika shughuli hiyo na kusema kuwa itakuwa ni kitu kizuri mno kwa wanawake kukutana na kujadili mambo mbalimbali pia kuangalia vitu vizuri vinavyofanywa na wanawake wenzao.

 

“Hakuna kitu ninakipenda kama kurudi nyumbani na kukutana na wanawake wenzangu mbalimbali na kujadiliana vitu vizuri hivyo ni vyema watu wangenunua tiketi zao mapema ambazo zinapatikana sehemu mbalimbali kama Zurii House of Beuaty na Malika Designer,” alisema Odemba.

Stori: Imelda Mtema, Dar


Loading...

Toa comment