The House of Favourite Newspapers

Odemba Studio kwa Diamond

0

STORI: BONIPHACE NGUMIJE NA IMELDA MTEMA | UWAZI| DAR ES SALAAM

Mwanamitindo maarufu Bongo na Miss Temeke 1997, Miriam Julius Odemba hivi karibuni alinaswa ‘mida mibovu’ katika ofisi za Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sinza Mapambano jijini hapa jambo lililoibua gumzo.

Kwa mujibu wa chanzo, mrembo huyo aliingia katika ofisi hizo saa 4 usiku na kupokelewa na wanamuziki kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’.

Miriam Odemba

“Miriam alipofika akiwa ndani ya gari kila mmoja alichukulia ni miongoni mwa wageni wanaotembelea ofisi hizo kila mara maana hatukumtambua, baada ya kushuka kila mmoja alibaki kinywa wazi na kujiuliza alikuwa amefuata nini ofisini hapo?

“Mara nyingi wanawake wengi wanaofika ofisini kwa Diamond hasa mida hiyo ni wale wanaosemwa kuwa na uhusiano naye kama, Hamisa Mobeto, Wema Sepetu enzi zile au mademu wa wanamuziki wake, akiwemo Jacqueline Wolper,” kilisema chanzo.

Rajab Abdulhan ‘Harmonize’.

Chanzo hicho kiliendelea kufunguka kuwa, baada ya mrembo huyo kuzama ndani ya mjengo wa WCB, nje aliacha gumzo watu wakimjadili huku wengine wakitaka kujua nini hasa kilimpeleka kwa Diamond usiku huo.

“Ukweli aliacha gumzo, watu walimjadili, maana kama ni masuala ya kazi si angeenda mchana! Kwa mazingira yalivyokuwa kwa vyovyote vile tulifahamu kuna kitu. Lakini hakukaa sana, akaondoka zake. Nahisi kwa sababu Diamond hakuwepo maana kuna muda tulimuona akitoka,” kilisema chanzo.

Baada ya Uwazi kuzinasa taarifa hizo kutoka kwa chanzo, Jumamosi liliamua kumtafuta Odemba ambapo alipatikana akiwa kwenye mazoezi yaliyofanywa na wakazi wa Wilaya ya Ubungo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ubungo Plaza na kufunguka:

Diamond na Salam.

“Ni kweli juzikati usiku nilikwenda WCB maana nilikuwa ninahitaji kuonana na meneja wa Diamond kwa ajili ya projekti yangu ya Run With Odemba lakini sikumkuta Diamond. Kama ningemkuta Diamond ni lazima ningepiga naye picha na watu wangeona kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuhusu uhusiano naye, hilo ni jipya kwangu, Watanzania waache kuunda mambo ambayo hayana maana na wasiyokuwa na uhakika nayo.”

Juzi Jumapili, Uwazi lilimsaka Diamond kwa lengo la kutaka kumsikia kama anaujua ugeni wa Odemba kwenye ofisi zake, lakini simu yake haikuwa hewani.

Leave A Reply