The House of Favourite Newspapers

ODEMBA AELEZA ALICHOAMBIWA NA KANYE WEST

Miriam Odemba

WADAU mbalimbali wa urembo nchini kamwe jina la mwanamitindo maarufu ndani na nje ya Bongo, Miriam Odemba haliwezi kutoka vichwani mwao kwa sababu ya kufanya vyema kwenye tansia hiyo.  Pamoja na shughuli ya urembo ambayo mpaka sasa bado anaifanya nchini Ufaransa,lakini ndio mwanamitindo wa kwanza kukutana na watu mbalimbali mashughuli duniani na kufanya watu wengi wajiulize nini siri ya mwanamitindo huyo ambapo aliweza kuifungua siri hiyo kupitia mahojiano maalum na Risasi Vibes kama ifuatavyo:

Risasi: Watu wengi wanashangazwa sana na nafasi ambayo unaipata kukutana na mastaa wakubwa duniani nini siri yako?

Odemba: Ni kweli kabisa unajua huku mimi nafanya kazi na kampuni kubwa inaitwa Urban, ambapo Fashion Show zao zinaalika mastaa wakubwa hivyo lazima nikutane nao.

Risasi: Mastaa wengi kama tunavyojua wanaongozana na mabaunsa wengi sana unawezaje kuwasogelea na kupiga nao picha tena za ukaribu zaidi?

Odemba: Ni kweli huwa kuna ugumu sana lakini kwa upande wangu wananijua na wengi wao hata nikiingia kwenye hafla zao unakuta wanavutiwa na mimi jinsi nilivyo mrefu na rangi yangu.

Risasi: Kuna picha ambayo ulipiga ukiwa na Kanye West, lakini walionekana mabaunsa wake wako pembeni wakikuangalia ilikuwaje mpaka ukapata nafasi ya kupiga picha naye?

Odemba: Yaani kuna Fasheni Show ambayo aliiandaa yeye mwenyewe sasa mimi nilikuwa mmojawapo kuna dizaina mkubwa nilikuwa navaa mavazi yake, baada ya kumailizika shughuli hiyo wakati naondoka nikamuona Kanye amesimama nikamfuata kumsalimia nikasema kwa nini tubaki nyuma kila siku nikamfuata alivyoniona akatoa bonge la tabasamu.

Risasi: Ikawaje sasa baada ya hapo?

Odemba: Alinikumbatia akaniuliza swali moja ambalo lilikuwa la kwanza kabisa nimetokea wapi? Nikamjibu akaniambia anapenda kunialika kesho yake kwenye After Party, ndipo nilipokutana naye tena.

Risasi: Ikawaje sasa?

Odemba: Baada ya hapo alikuwa ameshika shampeni yake mkononi akataka tushee na baada ya hapo alinifuata na kuomba kucheza na mimi kitendo ambacho kiliwafanya watu washangalie kwa sababu Kanye, alionekana wazi amechanganyikiwa kabisa.

Risasi: Kwa hiyo mlivyoondoka hapo mliendelea kuwasiliana au alikupa namba?

Odemba: Yaah,tuliendelea kuwasiliana na kipindi hicho alikuwa na Amber Rose lakini hata sasa hivi yuko na Kim,nilishawahi kwenda kuonana nao walikuja Paris.

Risasi: Ni vitu gani umejifunza baada ya kuonana na mastaa wakubwa kama hao?

Odemba: Ni vitu vingi sana, kwanza kumeniongezea kujitambua mno na ndoto zangu nyingi zimetimia kwa mfano leo ukimuuliza Naomi Campbell ananijua vizuri sana wala sio jina la kutafuta.

Risasi: Ila katika picha zako nyingi uko karibu sana na familia ya Kim Kadarshian, maana karibia wote umepiga nao picha,unazungumziaje hilo?

Odemba: Niko karibu sana na dizaina wao Olivia, ambaye sasa hivi anakuja vizuri sana na ndio maana mara nyingi napata nafasi ya kuonana nao.

Risasi: Haya Odemba nakushukuru sana kwa ufafanuzi wako mzuri.

Odemba: Asante na karibu na hata hivyo nimekuwa balozi kwenye kampuni kubwa ya Blac Up,hivyo bado nazidi kupepe rusha bendera yetu ya Tanzania.

Comments are closed.