Official Nai: Sijaachana na bwana’ngu!
BAADA ya kutupia video ya bwana’ake yenye viashiria kuwa wameachana, Video Vixen matata Bongo, Officiall Nai ameibuka na kusema hawajaachana. Bwana wa Officiall Nai aitwaye Moni kupitia ukurasa wake wa Instagram, hivi karibuni aliandika maneno haya ambayo watu waliyatafsiri kuwa tayari ameachana na mrembo huyo:
“Hapo zamani za kale ila wabongo nuksi jamani wana komenti yao inasema; mtaachana tu hadi yametimia. Daaah ila tulijitahidi miaka minne karibia.”
Baada ya maneno hayo kuzua gumzo mitandaoni, Mikito Nusunusu ilimtafuta Nai ambapo alipopatikana alifafanua: “Mimi mwenyewe nashangaa, sijaachana na bwana’angu sasa hayo maneno mimi siyaelewi nayaona tu mitandaoni kama wanavyoyaona wengine.”
STORI: NEEMA ADRIAN