OFISA MALAZI CHUO KIKUU (UDSM) ASEPA NA NDINGA YA TBL

Viongozi wa  kutoka Kampuni ya TBL wakichezesha promosheni inayojulikana kama ‘TBL Kumenoga” leo.

 

KAMPUNI ya TBL leo imemtangaza mshindi wa kwanza wa zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWDI, Julitha Kilawe, ambaye ni Ofisa Malazi kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya kuchezeshwa droo kweye promosheni mpya inayojulikana kama ‘TBL Kumenoga”.

 

TBL ilizindua promosheni hiyo inayojulikana kama ‘TBL kumenoga,Tukutane baa’ kwa lengo la kuwashukuru wateja wake na inafanyika kwenye baa mbalimbali nchini  ambapo washiriki wataweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWDI kwa kila mshindi wa droo kubwa ya mwezi na promoheni itafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia ilipozinduliwa mwezi uliopita.

 

Meneja  Udhamini na Mawasiliano ya Wateja TBL, David Tarimo, amesema promosheni hiyo itafanyika kupitia chapa maarufu za bia zinazozalishwa na kampuni ambazo ni Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.

 

Kwa upande wake, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli  amesema mbali na zawadi kubwa ya gari zipo zawadi nyingi za kujishindia kupitia promosheni hiyo ikiwemo bia za bure na kwamba promosheni hiyo itakuwa inafanyika wikiendi ambapo kila sehemu ya promosheni kutakuwepo bendera ya TBL Kumenoga.

 

Alisema ili kushiriki promosheni hiyo ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ anachotakiwa kufanya mteja ni kununua bia tatu za chapa zilizopo kwenye promosheni ambapo watapatiwa kuponi yenye namba ambazo wanapaswa kuzituma kupitia simu zao za mkononi kwenda namba 15451 kwa kutumia mitandao ya simu ya makampuni ya Vodacom, Tigo na Airtel.Wateja wenye mitandao mingine ya simu wanaweza kushiriki promosheni kupitia tovuti ya http://www.tblkumenoga.co.tz

 

 


Loading...

Toa comment