Ofisa Utumishi Tanesco Akutwa Gesti Akiomba Rushwa ya Ngono

TAASISI ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mtwara inamshikilia ofisa utumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Jumanne Songoro, kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mlalamikaji ambaye jina lake limehifadhiwa ili kumpangia majukumu mapya ya kazi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne, Julai 9, 2019, Kamanda wa Takukuru  wa Mtwara, Stephen Mafipa, amesema aliomba rushwa hiyo ili aweze kumpangia mlalamikaji majukumu mengine katika kitengo cha kudumu kulingana na kiwango chake cha elimu baada ya kubadilishiwa majukumu ya awali kufuatia maagizo kutoka Tanesco makao makuu.

 

 

Kamanda Mafipa amesema jana majira ya saa nane mchana walimkamata mtuhumiwa huyo kwani ni kinyume na kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 na kwamba atafikishwa mahakamani.

 

“Uchunguzi umebaini mtuhumiwa alianza kushawishi rushwa ya ngono kutoka kwa mlalamikaji kwa nyakati tofauti toka Disemba 2018 na ndipo Julai 4, 2019 mlalamikaji aliwasilisha malalamiko katika ofisi ya Takukuru mkoa tukafanya uchunguzi na baada ya kujiridhisha kuna mazingira ya rushwa tuliweka mtego na kufanikiwa kumkamata,” amesema Mafipa.

 

Amesema mtuhumiwa alikamatwa akiwa na mlalamikaji katika mojawapo ya vyumba vya nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Mtwara Mikindani akiwa tayari kutekeleza azma ya kupokea rushwa ya ngono.

 

MAJAMBAZI WAVAMIA MADUKA, WALINZI HAWAONEKANI HADI SASA!


Loading...

Toa comment