The House of Favourite Newspapers

Ofisi ya Zamani ya CCM Sengerema Kugeuzwa Kuwa Kitegauchumi

0
Mwonekano wa ofisi ya zamani ya Chama Cha  Mapinduzi (CCM) Wailaya ya Sengerema Mwanza.

 

Baada ya kumalizika kwa ofisi mpya ya CCM wilayani Sengerema imeleezwa kuwa ofisi ya zamani itakarabatiwa na kuwa kitegauchumi cha chama.

Hayo yamebainishwa leo jumamosi Oktoba 1 na Marco Makoye anayetetea nafasi yake ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.

 

Sambamba na hilo amesema kama wanaCCM kama watampatia tena lidhaa ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano atajenga ukumbi mkubwa wa biashara ambao utakuwa mali ya chama.

 

Makoye ambaye ameongoza CCM kwa kipindi cha miaka mitano amekuwa kiongozi wa vitendo kwa kukamilisha miradi ya chama sambamba na kuweka vitega uchumi ili chama kiweze kujitegemea.

 

Kwa kipindi cha uongozi wake amehamasisha ujenzi wa ofisi mpya ya CCM ambayo hadi sasa imekamilika na na kuanza kutumika sambamba na ujenzi wa vibanda vya biashara kwenye stendi ya mabasi mjini Sengerema.

Amewaomba wanaCCM wampatie ridha ya kukiongoza chama hicho katika uchaguzi unaotarajia kufanyika Oktoba 2 mwaka huu.

Kwa upande wake Samson Juma amesema chama kikiwa na viongozi bora wanaosimamia haki hakika kitasonga mbele kimaendeleo.

 

Naye  katibu wa CCM wilaya ya Sengerema Muhusini Zikatimu amesema siri ya mafanikio ya CCM ni umoja na ushirikiano uliopo baina ya wanachama na viongozi wake.

 

Viongozi ndani ya CCM wametakiwa kushirikiana na wanachama ili kusukuma gurudumu la maendeleo.

 

Leave A Reply