OFM YA MFUNGIA K AZI ‘DOGO’ WA MIL. 180

DAR ES SALAAM: TUHUMA za uhujumu uchumi zinazomkabili ‘bwa’mdogo’ Mustapha Kambangwa anayedaiwa kuiibia Serikali ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’, shilingi bilioni 188, zilizua maswali mengi miongoni mwa jamii.  

Moja kati ya maswali hayo ni kuhusu makazi yake yanayotajwa kuwa ni Kongowe nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo wengi walijiuliza inawezekanaje mtuhumiwa huyo akaishi huko wakati akidaiwa kuwa ni tajiri mkubwa. Kufuatia gumzo hilo Kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers kililazimika kuchimba makazi ya Kambangwa eneo la Kongowe lililotajwa katika utambulisho wake.

OFM kwa nyakati tofauti walizunguka sehemu mbalimbali za Kongowe, Mzinga, Goroka mpaka Tuwangoma, maeneo ambayo yanapakana Kongowe iliyotajwa na mtuhumiwa bila kuyaona makazi yake. Msako uliposhindwa kutoa majibu, timu ya uchunguzi ililazimika kubisha hodi ofisi za serikali za mitaa za maeneo hayo kwa ajili ya kuendeleza upepelezi wao.

 

NASSORO NJUWINE

Huyu ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kongowe ambaye baada ya kuulizwa kuhusu Kambangwa alisema; “Mimi ni mwenyeji tangu 1988 hivyo wote wanaokuja kupanga, kujenga au kuhamia maeneo haya wanapitia hapa ofisini, huyo Kambangwa angekuwa mkazi wa hapa Kongowe ningemfahamu.”

 

YAHAYA MOHAMMED

Huyu ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzinga B, eneo linalopakana na Kongowe ambaye alieleza haya: “Nimezaliwa hapahapa Mzinga miaka ya sabini, mpaka nachaguliwa kuwa mwenyekiti wa mtaa huu hii ni awamu yangu ya pili, hili eneo la Mzinga na Kongowe ni kama yameungana lakini huyo Kambangwa mnayetafuta makazi yake simfahamu kabisa.”

REHEMA SHAMTE

Mama huyu ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mzinga A, ambaye alisema: “Hapa Mzinga nimekuja mwaka 1990 huu ni mwaka wangu wa 29 maeneo ya Kongowe, Mzinga, Goroka, Tuwangoma yote nayafahamu vizuri na nafahamiana na matajiri mbalimbali wa maeneo hayo kupitia kazi yangu ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa na pia mimi ni dalali wa nyumba na viwanja lakini huyo Mustapha Kambangwa simjui, nimesikia tu kwenye vyombo vya habari kuwa anaishi huku.

 

ALLY KINDEWA

Kindewa ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mzinga B, na mkazi wa muda mrefu wa maeneo hayo.“Mimi ni mwenyeji hapa tangu mwaka 1978 nawafahamu watu wengi sana lakini huyo kijana simfahamu kabisa. Siamini kama anaishi huku.”

 

KAMBANGWA NI NANI?

Ni mfanyabiashara aliyetajwa kuwa ni mkazi wa Kongowe, Mbagala jijini Dar es Salaam ambaye mwishoni mwa mwaka jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kukwepa kodi na kujipatia Sh.bilioni 188.9 kupitia mashine ya kieletroniki (EFD).

Stori: Richard Bukos na Neema Adrian, Amani

Loading...

Toa comment