The House of Favourite Newspapers
gunners X

Ohooo! Serikali Yamweka Sanchi Kikaangoni

0

KUTOKANA na skendo ya picha zake chafu zilizosambaa mitandaoni na kuzua gumzo la aina yake, serikali imemuweka kikaangoni mwanamitindo mwenye shepu ya aina yake Bongo, Jane Rimoy, ‘Sanchi’ Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili.

 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa ‘Basata’, Godfrey Mngereza alisema wapo kwenye maandalizi ya kukaa kama viongozi ili kutafuta mwarobaini wa kilichofanywa na Sanchi.

 

Aliendelea kusema kuwa video hizo chafu zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita, wako kwenye majadiliano kama viongozi ili wajue ni nini cha kufanya.

“Leo (Jumatatu) ndiyo tumeingia ofisini muda si mrefu, kwa hiyo nasubiri nikae kikao na wenzangu halafu ndiyo tujue ni hatua gani tutachukua kwa Sanchi ili asije akarudia tena,” alisema Mngereza.

 

ILIKUWAJE?

Wiki iliyopita Video chafu za Sanchi zilisambaa kwa kasi ya aina yake kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha gumzo kubwa kwa watu wakilaani kwamba je, wazazi wake wanajisikiaje hasa mama yake maana alichofanya siyo sawa kimaadili.

 

KUMBUKUMBU

Hii siyo mara ya kwanza kwa Sanchi picha zake chafu kusambaa, kwani zilishasambaa tena na kuitwa na serikali lakini hajakoma ndiyo maana zimesambaa tena kwa mara nyingine.

SANCHI ANASEMAJE?

Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Sanchi ili aelezee ilikuwaje, lakini simu yake haikupatikana hewani lakini kuhusu ishu hiyo, aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram na kutoa ufafanuzi ufuatao;

“Sikutaka hata kuaddress hili jambo lakini nimeona linakuwa kwa kasi sana. Let me say this clearly hizo video mnazotumiana huko WhatsApp SIO MIMI.

 

“Jamani msinifananishe na shepu za kawaida mnanikosea. Yani sijaumbwa hivyo. Take your time kuchunguza utajua tu. Wala hutotumia nguvu nyingi kujua hizo video siyo mimi. Details kidogo tu.

 

“Kuna video nimeona mdada amelala kwenye jakuzi jamani hiyo siyo shape yangu. Hiyo shape ni ndogo mnooo. Mimi ningelala hivyo ingekuwa hatari ningesambaa sana manake nimejazia zaidi. Jakuzi zenyewe huwa sitoshei nakaa kiupande. Rangi yake pia siyo kama yangu. Na maziwa yangu yamejaa zaidi siyo kama hayo.

 

“Sitetereki wala sitoyumbishwa. Kwa wanaojifariji kusema ni mimi darlings am sorry to disappoint you it ain’t me. Nimeposti hili kwa ajili ya watu ninaowapenda wasije kuamini uongo.”

STORI: NEEMA ADRIAN, RISASI

Leave A Reply