The House of Favourite Newspapers

Okwa, Chama Wanogesha Kombinesheni ya Zoran Simba, Wawatambia Yanga

0

KOCHA Mkuu wa Simba Mserbia, Zoran Maki amefurahishwa na muunganiko wa viungo wake wawili Mzambia Clatous Chama na Mghana Augustine Okwa.

 

Hiyo ikiwa ni dakika chache mara baada ya mchezo wa kirafaki wa kimataifa uliochezwa juzi Jumatatu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam shisi ya St George ya nchini Ethiopia.

 

Mchezo huo ulichezwa katika kunogesha kilele cha Simba Day ambacho ufanyika kila mwaka kabla ya kuanza msimu mpya ambao utumika kutambulisha wachezaji.

Akizungumza na Championi Jumatano, Zoran alisema kuwa alifuraishwa na mabadiliko aliyoyafanya katika kipindi cha pili kwa kuwaingiza viungo wake Chama, Okwa na Victor Akpan.

 

Zoran alisema kuwa kuingia kwa viungo hao kipindi cha pili kulibadili mchezo na kuitawala safu ya kiungo ya St George ambao kipindi cha kwanza walicheza kwa kuelewana na kuwashambulia.

 

Aliongeza kuwa muunganiko huo wa viungo umemshawishi kuendelea kuwatumia wachezaji hao ambao Okwa alifunga bao la pili akiunganisha krosi nzuri ya Chama.

“Kipindi cha kwanza wapinzani wetu walitawala katika safu ya kiungo, lakini mabadiliko niliyoyafanya kipindi cha pili kwa kuwaingiza viungo wangu Okwa, Chama na Akpan kuiimarisha safu hiyo.

 

“Walivyongia viungo tulifanikiwa kutawala safu hiyo ya kiungo kwa kucheza soka la pasi za haraka tukienda katika goli la wapinzani wetu.

 

“Nataka kuona wachezaji wangu wacheze soka la aina hiyo, pia wazoeane haraka wakati tukielekea katika mchezo unaofuatia wa Ngao ya Jamii,” alisema Zoran.

Leave A Reply