The House of Favourite Newspapers

Okwi Aanza Kuwindwa Kimyakimya

0
Mshambuliaji wa Em­manuel Okwi.

 

STRAIKA wa Simba, Em­manuel Okwi, raia wa Uganda, kwa sasa ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu Bara, lakini wap­inzani wake wameanza kumuwinda kimyakimya wakitaka kumpiku.

 

Miongoni mwa wanaojipanga kwa ajili ya kumpiku Okwi ni straika wa Singida United, Danny Usengimana na yule wa Prisons, Mohammed Rashid.

 

Ikumbukwe kuwa, kabla ya mechi za jana Jumapili za ligi hiyo, Okwi alikuwa kileleni mwa ufungaji akiwa na mabao nane, akifuatiwa na Mohammed Rashid wa Prisons aliyefunga mabao sita.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Usengimana alisema: “Nahitaji kuwa bora kila siku, ili kufanikisha hilo, nimekuwa nikifanya mazoezi ya nguvu kuhakikisha nafikia malengo niliyojiwekea.

 

“Nimejipanga kweli kuona naendelea kufunga mabao kadiri niwezavyo, lengo likiwa ni kumaliza msimu nikiwa kinara na kuibuka na tuzo ya ufungaji bila ya kujali ushindani uliopo sasa.”

 

Naye Rashid alisema: “Nitafurahi kama nikiibuka kuwa mfungaji bora msimu huu, kuwa nyuma ya kinara kwa mabao mawili wala hainipi shida sana, nitaendelea kupambana kuhakikisha nafikia malengo yangu.”

Stori: Omary Mdose, Championi

Leave A Reply