The House of Favourite Newspapers

OKWI ATUA KISTAILI ZENJI

Emmanuel Okwi.

STRAIKA kipenzi cha mashabiki wa Simba, Emmanuel Okwi jana Jumatano alitua kwa ndege mjini Zanzibar huku wachezaji wenzie wakipanda boti. Simba itacheza mechi yao ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi kesho Ijumaa dhidi ya Chipukizi usiku mjini Unguja huku Kocha Patrick Aussems akipangua kikosi chake.

Okwi ambaye ni raia wa Uganda, kwa miaka kadhaa sasa amekuwa hatumii usafiri wa maji Simba inapokwenda Zanzibar kwa maelezo kwamba anaogopa maji na hawezi kuvumilia, jambo ambalo linaulazimu uongozi kumkatia tiketi ya ndege.

 

Mechi hiyo ya Chipukizi inatazamiwa kuwa na ushindani wa aina yake kutokana na sura mpya ambazo zitaingizwa kwenye kikosi cha Simba ambacho kinajiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Chipukizi wamekuwa wakifanya vizuri katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kuwa na damu changa. Timu tisa zitashiriki michuano hiyo, sita kutoka Zanzibar ambazo ni KVZ, KMKM, Jamhuri, Chipukizi, Mlandege na Malindi. Za Bara ni Azam, Simba na Yanga.

 

Kundi A linajumuisha Chipukizi, Mlandege, KMKM na Simba wakati Kundi B imo KVZ, Malindi, Jamhuri, Azam na Yanga. Kwa mujibu wa kamati ya maandalizi ya zawadi kwa mshindi wa kwanza itaongezwa kutoka Sh10milioni hadi Sh15milioni sambamba na medali za dhahabu pamoja na kombe. Mshindi wa pili atapata Sh10 milioni 10.

Azam ndio wamekuwa wakifanya vizuri katika miaka ya hivi karibuni kwenye michuano hiyo kwani wamebeba kombe hilo mara mbili mfululizo

LUNYAMADZO MLYUK

Comments are closed.